Dr. Nduka Dental Clinic - Moshi

Dr. Nduka Dental Clinic - Moshi

DR. NDUKA is dental specialist, was regional dental doctor at mawenzi hospital - moshi (RDO) studied Russia. Welcome for our service. Over 35 years experience in Dentistry.

We use latest technologies to make you smile

Operating as usual

If you've exhausted all your options to break the thumb sucking habit and your child has still not kicked the habit, see your orthodontist about getting a device fitted.
Beware of oral habits! They may be a reason to your child's crooked teeth.

Ikiwa umechoka chaguo zako zote ili kuvunja tabia ya kunyonya kidole kwa mtoto wako bado hajakataa tabia hiyo, angalia mtaalamu wako kuhusu kupata kifaa kilichofungwa.
Jihadharini na tabia za mdomo! Wanaweza kuwa sababu ya meno kuwa na shape mbaya ukubwani.

[09/08/16]   DR. NDUKA DENTAL CLINIC SERVICE - MOSHI

1. UCHUNGUZI WA KINYWA NA MENO (DENTAL CHECK UP)

2. KUZIBA MENO ( TOOTH FILLING)

3. KUSAFISHA MENO (SCALING AND POLISHING)

4. KUBADILI MENO YA RANGI KUWA MEUPE ( VENEER)

5. KUUA JINO (ROOT CANAL TREATMENT)

6. HARUFU MBAYA MDOMONI ( BAD BREATH)

7. MENO KUTINGISHIKA (LOOSE TEETH)

8. KUVUNJIKA KWA TAYA (FRACTURE OF THE JAW)

9. KUWEKA MENO YA BANDIA YA KUVUA (REMOVABLE DENTURES)

10. MENO YA BANDIA BILA KUVUA (FIXED DENTURES)

11. KUPANDIKIZA MENO BANDIA (DENTAL IMPLANT)

DR. NDUKA DENTAL CLINIC IS PREPARING A COMPREHENSIVE DENTAL CARE TO THE COMMUNITY....

YOURS IN PUBLIC SERVICE,
DR. NDUKA
SPECIALIST OF DENTAL CLINIC

TUKO MOSHI MJINI BARABARA YA KAWAWA

FOR MORE INFORMATION CONTACT:

MOBILES: 0658829028

KUTOBOKA KWA MENO NI NINI?
Kutoboka kwa meno ni ile hali ya jino au meno kutengeneza tundu ikiwa ni matokeo ya asidi (tindikali) izalishwayo na bakteria baada ya mtu kula vyakula vyenye sukari

Nini Kinasababisha Meno Kutoboka?
Meno kutoboka husababishwa na utando asidi (tindikali) izalishwayo na bakteria walioko kwenye utando mlaini ambayo taratibu huweza kutoboa jino husika kwa kuanzia kwenye enameli na kuzidi kuingia ndani zaidi. Kutoboka kwa jino huharibu jino husika ambalo lisipozibwa mapema huweza kuishia kung’olewa.

Enameli Ni Nini? (What is enamel?)
Enameli ni gamba gumu linalofunika jino na ndilo sehemu unayoiona kwenye meno ya mtu yeyote yasiyo na tobo gamba hili ndio kitu kigumu zaidi kuliko chochote katika mwili wa mwanadamu na halina mishipa ya fahamu,damu wala halina hisia za maumivu.

Dentini Ni Nini? (What is dentine?)
Dentini ni gamba la katikati kwenye jino lililoko baada ya enameli, hili ndilo huchukua sehemu kubwa ya jino na kwakua lina na mishipa ya fahamu lina hisia za maumivu. Dentini ndio gamba lililfunika moyo wa jino (pulp).

Je Moyo Wa Jino Ni Nini? (What is the pulp?)
Moyo wa jino ni sehemu laini ya jino ambayo iko katikati kabisa mwa jino na ambyo ina mishipa ya fahamu na mishipa ya damu.
Kwanini Meno Yangu Yanatoboka?
Meno hutoboka wakati sukari iliyopo kwenye chakula inapotumiwa na bakteria walioko kwenye kinywa ambao kisha hutengeneza tindikali (asidi). Kila mara ulapo ama unywapo vitu vilivyo na sukari, tindikali hii hushambulia meno na taratibu huweza kuyatoboa. Mashambulizi haya huweza kuchukua hata saa moja baada ya kuwa umekula vitu vya sukari, kabla ya madini ya chumvi yaliyoko kwenye mate kupambana na hali hiyo. Ikumbukwe kuwa si sukari tu ambayo ni tishio kwa meno yako, hata vyakula vya wanga navyo ni hatari kwani vinaposagwa huweza kutoa sukari ambao nayo huchangia kuozesha meno.
Hivvo basi kutumia vyakula na vinywaji vya sukari kati ya mlo mmoja na mwingine huongeza uwezekano wa kutoboka meno kwani meno husika huwa yanashambaliwa muda wote na yanakosa muda wa kupumzika. Hivyo ni muhimu kujiepusha na matumizi ya vyakula na vinywaji vya sukari kwa siku nzima.

Je Ni Zipi Ni Dalili Za Jino Lililotoboka?
Kwa kawaida kwenye hatua za awali za utobokaji wa meno huwa hakuna dalili yeyote, isipokuwa jino husika huweza kuwa na alama nyeupe kama ya chaki kwenye eneo ambalo linaanza kutoboka. Alama hii huonwa na daktari wa meno anapokuchunguza ama anapopiga mionzi jino husika. Ndio sababu tunasisitiza ni vizuri kumuona Daktari wa kinywa na meno mara kwa mara, tundu dogo ni rahisi kulitibu kuliko tundu lililo kubwa.

Nini Kinatokea Kama Nina Tundu?
Mara tu tundu lililoko kwenye jino linafika kwenye sehemu ya kati ya jino (dentine), jino huanza kuwa na maumivu hasa unapotumia vitu vya baridi au moto, vitu vya sukari ama vya asidi (tindikali).

Nini Kitatokea Kama Sitatibiwa Mapema?
Maumivu ya jino ni dalili kwamba unatakiwa ukamuone Daktari wa kinywa na meno haraka, kwani hiyo huwa ni taarifa kwamba kuna tatizo. Kama usipozingatia madhara yatakua makubwa na inawezekana ukapoteza jino husika ambalo lingeweza kuokolewa kama ungewahi.

Je Ni Maeneo Yapi Ya Meno Huweza Kutoboka Kwa Urahisi?
Maeneo ya kutafunia chakula na maeneo kati ya jino na jino ndio maeneo rahisi zaidi kutoboka, hii ni kwa sababu mabaka ya vyakula na utando mlaini (Plaque) huweza kujishika katika maeneo haya. Lakini kwa ujumla maeneo yote ya meno huweza kutoboka.

Je Nitahitaji Matibabu Ya Aina Gani?
Daktari ataondoa sehemu ya jino iliyooza/toboka na kuweka dawa maalumu ya kujaza eneo husika. Wakati mwingine tundu huwa ni kubwa kiasi cha kuifikia mishipa ya fahamu ya jino husika, inapofikia hapo Daktari huweza kufanya matibabu ya mzizi wa jino ili kuweza kuhakikisha kwamba unaendelea kuwa na jino lako na kulitumia. Na inapotokea kwamba jino lako limetoboka sana kiasi cha kutoweza kukarabatiwa Daktari huweza kushauri kwamba litolewe.

Je Ni Mara Zote Nitahitaji Kuzibwa Meno?
Hapana. Katika hatua za mwanzoni kabisa kama umewahi Daktari huweza kuweka kwenye jino linaloanza kutoboka dawa maalumu (fluoride varnish), ili kuweza kusaidia kurudishia madini yaliyopotea kwenye meno. Japokuwa ni muhimu kufuatisha mapendekezo ya daktari wa kinywa na meno kuhusu namna ya kujizuia kulingana na hali yako, ili yasianze kutoboka tena.

Je Ninaweza Kufanya Nini Ili Kuzuia Kutoboka Kwa Meno?
Njia bora kabisa ya kuzuia kutoboka kwa meno ni kwa kupiga mswaki vizuri na meno yote usiku kabla ya kulala na pia siku Inayofuata asubuhi baada ya kula kwa kutumia dawa ya meno yenye madini ya floridi. Hakikisha kwamba unayafikia maeneo yote ya meno wakati wa kupiga mswaki. Fanya flosi ili kusafisha sehemu finyu za kati ya meno ili kusafisha sehemu hizo. Hizi ni sehemu ambazo mswaki wa kawaida haufiki

Je kuna kitu Chochote Cha Ziada Ninachoweza Kufanya?
Mtembelee Daktari wa kinywa na meno mara kwa mara, kadiri atakavyopendekeza. Punguza milo ya sukari na tindikali. Jiepushe na vyakula vya sukari katika milo yako ili kupunguza muda ambao meno yako yatakua yanashambuliwa na tindikali.
Kutafuna jojo zisizo na sukari mara tu baada ya kula husaidia matezi kuzalisha mate zaidi na hivyo kufanya tindikali izalishwayo kuondolewa kinywani na mate hayo
Kama una maswali ama unahitaji ushauri zaidi binafsi, tafadhali usisite kuwasiliana nasi katika clinic yetu iliyopo moshi mjini au piga simu 0784829028 au 0658829028

Dr. Nduka Dental Clinic - Moshi

Dr. Nduka Dental Clinic - Moshi's cover photo

Dr. Nduka Dental Clinic - Moshi

Want your business to be the top-listed Dentist in Moshi?

Click here to claim your Sponsored Listing.

Location

Telephone

Address


P.O.BOX 6691
Moshi
Other Moshi dentists (show all)
Zähne für Afrika Zähne für Afrika
Uchira
Moshi

Zähne für Afrika - teeth for africa

Moshi Dental Clinic Moshi Dental Clinic
Shanty Town
Moshi

Moshi dental clinic is the private Dental Clinic offering all types dental services . we are located inside Moshi Arusha hospital in Moshi Town

About   Privacy   Login C